Jumamosi, 3 Septemba 2016

De 25

Gangstar noma
By: benchrys
25

.......nilipotazama niliweza kuona namba ya god yule aliyekuwa mmbea wa darasa maarufu kwa jina la facebook licha ya kuwa yeye halitaki. Nilipokea simu yake na kutulia kimya, yaani niliuweka uwe kama mchezo kwa kila atakaepiga simu kwangu, baada ya god kuona siongei ikamlazimu aanze kuongea mwenyewe
   Oya been vipi nambie
  Nikwambie nini atha na wewe fb
  Halafu hilo jina mwanangu staki mm
  Sio utaki sema tu uache mishe za ki fb fb vip wewe, haya unasemaje paparazi langu.hii kauli ilimchoma sana god hadi alikata simu mimi nikabaki nacheka tuu pekeangu baada ya dakika moja tena simu iliita niliipokea lakini aliyekuwa akiongea sikumwelewa hata kidogo maana sauti yake ilikuwa ya mkwaruzo sana na sikufanikiwa kumjibu chochote maana maongezi yake alikuwa akifoka tu
Aliongea sana kisha akakata ile simu nikabaki najiuliza maswali mengi tuu kwamana sikumuelewa anachokisema halafu anafoka balaa

Nkiwa home
..ivi wewe ben unatafuta matatizo watakuja kukuteka hao watu sijui mwenyewe kama unahisi unachokifanya kipo powa sana shauri yako...yalikuwa ni maneno ya naomi sijui alipata wapi habari za kuwa nimepiga watu huko, sikutaka kumwuliza ni kwanini anasema maneno kama hayo mana nilijua wazi kwamba ntakuwa nachochea mdomo wake kwa sababu ben kiufupi sio mtu wa maneno sana na ndio asili yangu hivo nilivo toka mdogo
..e bana kama wataniteka powa ila sitakubali nichunguzwe kijingajinga hivihivi sawa naomi baada ya kuongea vile nilinyanyua simu na kumpigia joel
..oya joh nambie wapi engo
..nipo tuu kihome ukowapi wewe
..road nakuja mitaa yenu
..powa mdau utanikuta mi npo tyu
..ok sio muda basi(simu ilikatwa)
Niliianza safari ya kwenda kwa joel lakini nikiwa nakata kona katika chochoro fulani nilivutwa shati langu hadi kishikizo kilikatika halafu nikabanwa ukutani huku nikionyeshewa kisu shingoni duuh nilizungusha akili fasta namna ya kujitoa lakini kila staili niliyotafuta niliona kama utanidhuru. Alikuwa mdada fulani mrefu kiasi ambaye alivalia vazi la kiislam huku akiwa amejiziba kila kona ya mwili wake mana hadi usoni alivalia miwani yenye rangi nyeusi ambapo nilijitahidi kumwangalia lakini sikuweza kumtambua hata kwa kutumia signal ya macho kwa sababu alinitingia na ile miwani
,,ivi wewe ndio dogo wa kunyanyasa watu hapa mtaani si ndio. Aliniuliza hivi kisha nikamjibu jeuri
,,kwani umeona nimemwibia mtu yeyote hadi useme nawanyanyasa, baada ya mimi kusema vile akawa kama anashika kile kisu vizuri, nikaja kugundua kuwa aliwekea upande ambao hauna makali hapohapo sikuzubaa nilimpa kufuti cha tumbo hadi akaanguka chini kisha nikanyang'anya kile kisu baada ya kuona hawezi kunyanyuka nilimfuata nikamvuta na kunsogeza pembeni ya kile kibarabara huku nikijisemea kama ni makosa bora iwe tuu kisha nikamvua ile miwani nikashituka kuona ni sura kama ya kiume nikajipa moyo nikamtoa na lile hijabu hapo ndio nilithibitisha kuwa ni mwanaume nilipomuangalia nilikumbuka kwamba ni yule ambae nilimpiga ile siku nilipotoka uwanjani nikiwa narudi nyumbani kwa merry, baada ya kugundua vile sikudili nae niliendelea na safari yangu ya kwenda kwa joel huku najiuliza maswali ivi mwanaume anawezaje kutumia sauti ya kike kama vile ila sikupata jibu na baada ya mda mfupi nikawa nipo kwa joel nyumbani..
Oya joh nishafika fungua mlango niliongea vile joel akaja hadi mlangoni na kunifungulia mlango niliingia ndani tukasalimiana lakini baadae joel akapoa ghafla akawa anaongea kinyonge hadi nikajiuliza kisha nikamuuliza na yeye unamatatizo mbona upo hivo?
Hakunijibu ila niligundua kilichomfanya apoe kumbe mkononi nilikuwa bado na kile kisu baada ya kugundua vile nilimpa na kumwambia akiweke hicho kisu,, alikipokea na kukiweka ndani
....baada ya hapo stori ziliendelea vizuri muda ulisonga nikamuaga kuwa narudi nyumbani niliondoka mdogomdogo. Nikiwa njian simu yangu yangu iliita niliitoa mfukoni ila nilipoangalia niliona ni namba ngeni sikuipokea nikarudisha mfukoni nilitembea hadi nafika nyumbani bila janga lolote kwa upande wangu baada ya kufika salama nilimshukuru Mungu maana kila ninapopita sikosi mkosi,, nilipofika nyumbani nilifuata maji nikaoga bila kujali yamoto au ya baridi.

    
Na leo ushaleta majanga yako yani we sijui kimekupata nini. Aliongea maneno hayo naomi
///naomi hayo majanga sisababishi mimi ivi labda nikuulize mtu akija na kukupiga kofi hadi unaangusha mchozi na uwezo wa kumjibu unao utamuacha au utajibu. Nilimjibu hivo nae akasema nimuache mimi yesu toa kisu natoa panga dadeki. Baada ya kunijibu hivo nilicheka kisha nikampa swali tena "sasa kama kwako wewe ipo hivo mimi itashindikaneje atha au mimi ndio yesu acha kunimaindi hivo bhana vp wewe"

Baba na mama walirudi toka kazini kwao iliingia giza tulikula tukapiga stori chache na kwenda kulala...nikiwa nimelala

****Oya mwanangu dogo mwenyewe ndio yuuuule sasa twende tukamnyake mapema kabla hajashutukia ishu sasa sio kuharibu na leo mwanangu..
Powa hapa hakiharibiki kitu jembe langu we twende ila wewe pita huku na mimi napita huku ole wako na wewe uharibu(Safari ilianza)
Dadeki shika mikono hiyo huyu boya leo wetu na nilivo na hasira nae sijui ntakacho mfanya..powa nshafunga hiyo kamba kawashe gari twende zetu dadeki mpuuzi wewe..
******kumbe ilikuwa ni ndoto nilishituka usingizini kwaajili ya ile ndoto duuuh sikuamini nilichokiona mbele yangu...itaendeleaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni