Jumapili, 28 Agosti 2016

De 20

Gangstar noma
By: benchrys
20

.niliipokea ile namba ngeni ambayo ilikuwa ikiita kwa ule mda ndipo nikaja kusikia sauti ya mtu wakiume ambae hata nilipojaribu kuvuta hisia ili niigundue sauti ile ni ya nani sikuweza kuigundua kabisa alikuwa akiongea mada ambazo kwa akili yangu niliona tuu ni kama  ananipotezea mda wangu kwa yale mambo ambayo alikuwa akiyaongea
;;;oya nakusikia mda wote kunifosi nikwambie maeneo ambayo mimi nipo shida yako nini nawewe ni nani mbona sikusomi mkuu!!!!!
;;;;;ahaaa mwanangu ben ee unazingua inamaana hii sauti huigundui kabisa au nsio lengo lako uniyeyushe acha kuzingua bhana uko wapi wapi wewe mimi nataka tumeet now mkuu au mimi ninanoma na wewe,,,,
;;;;;;kudadeki zako kama hujielezi na mimi nakata simu yangu mana unanimalizia tuu chaji na sina aina ya umeme wa aina yeyote huku so acha kuzingua we nani?
       Nilijitahidi kumwuliza yeye ni nni lakini hakuweza kunitajia jina lake ni nani na hata angenitajia ningejua kwamba tayari huyu ni mwongo baada ya kuongea hayo bila mafanikio ya kumjua yeye ni nani nikaona isiwe shida hata kidogo sikupoteza mdfa hata kidogo nilikata simu kisha nikamalizia kupata chakula na kwenda kuendelea na yale mazoezi ya kupasua yale maboga nilitumia nguvu kujirusha kama babu alivo fanya mara ya kwanza hadi akapasua niliweza kupasua boga moja nikarudia mara nyingi nikaweza kupasua boga na la pili baada ya hapo nikawa na uzoefu maana niliweza kupasua yale maboga kumi na zaidi ya yale aliyo nambia babu niyapasue baada ya hapo nikaanza kuondoka kwenda upande wa ile miti kabla sijafika mbali nikasikia mtu akipiga makofi ishara ya kushangilia niligeuka nyuma ndipo niliweza kumwona babu akishangilia akasema nadhani sasa umeweza hatu aya kwanza hongera sana ok hatua inayofuata nenda kwenye miti sasa na ujitahidi kuvunja nitakuwa na zawadi kwaajili yako ukiweza kila kitu vizuri alimaliza hivo kisha mimi niliondoka pale
       Huu mda niliipiga ile miti kwa nguvu sana na kwa hasira ya kupata ile zawadi ambayo babau ameniahidi kwamba atanipa kama nitaweza kupatia kila atakachonifunza nijitahidi kwa jihudi zangu kupiga hii miti lakini niliweza hatua ndogo tuu ya kuutikisa mti kwa ngumi nikajitahidi kuongeza nguvu zangu lakini nilikuwa tayari nimeshachoka nikataka niangalie mda ni saa ngapi nikakumbuka kuwa simu niliiacha kuondoa usumbufu basi nilijifunza hadi inaingia jioni ndio nilirudi nyumbani nikiwa nimechoka vibaya tulikula chakula cha usiku tukalala lala

*********************

Asubuhi nilishitushwa na mlio wa simu yangu maana jana nimelala kama mzoga vile kwakuwa sikuzoea kufanya mazoezi hata kupiga pushapu
Nilikurupuka toka nilipolala na kuifuata simu ilipo kisha nikaipokea baada ya kuona ni namba ya merry ikipiga

;;;;hallo ben vipi!!
;;;;safi tuu za huko sister
;;;;huku kupo fresh sema tuu wanakusaka bado sijui wana nini hawa watu
;;;;aaaaa waache wanitafute tuu wakijisikia kuacha wataacha
      Niliongea hayo na merry kisha nikanawa uso na kuendelea na mambo mengine kiufupi niseme katika kuishi na huyu babu shughuli yangu kubwa ilikuwa ni mazoezi na siyo swala jingine niliizoea hali hiyo pia niliendelea kufundishwa mazoezi mengi zaidi baada ya hapo nikawa tayari nipo vizuri ilichukua muda kama wa mwezi mmoja hivi ndipo babu aliponiambia ben saiz unauwezo wa kuondoka hili eneo ila kama ukijisikia unaweza kunitembea lakini nitakuomba kama unakuja unipe taarifa ya kwamba unakuja kunitembelea sharti ukiniona huko mjini kwenu usje jaribu kuniita mwalimu tena na  hata ukiniona jifanye hata hunijui kabisa maana sihitaji mtu yoyote ajue haya mambo niliyokufunza huku kwenye eneo langu la siri na ndio maana sikutaka hata kukwambia hili eneo linaitwaje isipokuwa kajifunze kusoma ramani za maeneo kadhaa kupitia computer pia jitahidi kuwa mdukuzi lakini mwenye break na mambo ambayo anayoyafanya

*****baada ya babu kuongea yale yote akanionyesha mtumbwi ambao naweza kutumia ninapoondoka kurudi makwetu halafu akanikabidhi kisu fulani chenye urefu kama vile vya maninja lakini sikuona ajabu maana hivo vyote alishanifundisha jinsi ya kuvitumia kwa  kupambana kisha akanikabidhi kitu kama kisu na kuniambia humu unaweza kutunzia dawa zako unazotumia ila nimekuwekea chache humohumo mwisho akanipa kitu fulani kama karatasi na mkoba fulani mzuri kweli akanambia hili karatasi tumia njia zote unazojua mtu asilione hata kwa bahati mbaya nilimwitikia babu kisha tukapeana ishara na mimi nikaanza kuufuata mtumbwi alionionyesha na kuongoza nao kwenye ule mto wenye mamba,,, taratibu nikaanza kufuata njia kurudi kule nilikokutana na babu sikuweza kupatwa na jambo lolote hadi nilipofanikiwa kufika hapo nilishuka na kuanza kuzitafuta njia za kunifikisha nyumbani kwa merry lakini nikaona itakuwa sio vyema kama ikitokea naenda kimyakimya bila kumshitua kwenye simu nilinyanyua simu yangu na kuitafuta namba ya merry na kuipiga aliipokea kwa haraka na kuniuliza vipi umerudi nini nilimwambia ndio nimerudi upo wapi saizi akanambia hayupo nyumbani ila alinielekeza mahali ambapo ameziweka funguo na mimi nilikata simu na kuelekea nyumbani kule lakini kabla sijakamata njia vyema ndipo niliweza kumwona kijana mmoja hivi aliyekuwa akiongea na mwenzake niliposikiliza sauti nikakumbuka huyu ndiye aliye nipigia simu ili kuhakikisha nilichukua simu yangu na kupiga ile namba simu ilianza kuita kwake pale akapokea kwa shobo yap ben engo zipi mdau wangu nilimwambia kwa sauti ya chini nyuma yako akageuka na kuniona mimi ben huku nikiwa na begi fulani lefu akataka kujifanya anajua ubabe akaniamrisha ben dadeki sisi tunasanda kufanya kazi za watu kukutafuta halafu wewe unakula bata tuu na mabegi kama hayo hebu lilete mda wote nilikuwa nikimwangalia tu,,, nae hakuzubaa akanisogelea na kutaka kuvua begi, nikaona sasa huku ni kuzoeana nilifutuka na kumpiga na bonge la teke la kifua alianguka chini huku akikohoa kwa shida hapo na mimi nikaendelea na safari zangu

*******nilifika hadi nyumbani kwa merry mda mfupi tuu ndipo nikatafuta chakula mahali aliponielekeza kipo nilikila kwa fujo kweli mana nilikuwa na njaa ya safari ya kusafiri kwenye maji yale zoezi halikuchukua muda mrefu sana na baada ya hapo nilielekea kule kwenye chumba changu ambacho nilipewa pindi nafika kwa merry siku ya kwanza nilikiona kama nilivokiacha moja kwa moja nikanyosha kuelekea kwenye computer ili kuendelea kujua mambo zaidi ya yale ninayo fahamu muda ulienda merry nae akawa amerudi nyumbani tulisalimiana tukaendelea na mambo yanayotakiwa iliingia mara masaa nayo hayakukaa nyuma yakawahi ikaingia jion merry aliwasha tv ili tuweze kusikia hata taarifa ya habari japo kwa ufupi wote tulitulia ili kusikiliza
****familia moja imevamiwa na kuporwa kiasi na mali nyingine habari zinaonyesha kwamba……… sikutaka hata kusikiliza sana baada ya kuona ni nyumbani kwetu niliingia kulala kwa hasira ili siku yapili nijiandae kwenda nyumbani kwetu ambako ndio kwa baba na mama nililala lakini niliona kama usingizi hauji kibaya nikahisi kama hata saa kuna mtu anaichezea ili ichelewe kuumaliza usiku huu ila baada ya muda mrefu sana nilipitiwa na usingizi kwenda wapi tutajua mbeleni,,,, lakini kabla usingizi haujakolea vizuri simu yangu iliita nilipo ipokea ikazima shit!!! Kumbe sijaichaji niliiweka simu chaji kulala***asubuhi ilipofiika nilianza safari yangu kwenda nyumbani lakini nikiwa njiani……itaendelaaaaaaaaaaaaaaa

Benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni