Jumapili, 28 Agosti 2016

De 18

Gangstar noma
By: benchrys
18

.........mkuu wao alikuwa tayari yupo chini akiwa anatoa povu mdomoni akiwa hajielewi kabisa..basi baadhi yao walimchukua na kumwingiza kwenye gari kwaajili ya huduma ya kwanza huku wengine wakijiandaa kuanza mashambulizi dhidi ya merry lakini merry nae hakuwa zoba maana anawaza mbali kama draft dume kwenye computer wakati wao wakijadiliana kuwa wamshike ili wampe kipigo kitakatifu na yeye alikuwa akipiga hesabu namna ya kuwatoka na kuwapa adhabu na kuwashikisha adabu mipango walivokuwa wakiipanga
::::::::::majambazi:::::
Oya wadau huyu dada asituletee miyeyusho kama mnavoona kichaa wetu tayari yupo chali hapa na sisi kukimbia haitakiwi lazima ajue sisi ni akina nani tumpe kisago cha kutosha baadhi yetu mtamkamata na wengine watakuwa na kumpa kipigo cha maana tuu..........

::::::::merry:::::::::
Duuh ivi hapa bila mimi kujiongeza wanaweza niua mana hadi hii hatua sijajua wanawaza nini kwenye vichwa vyao kwa hichi kitendo nilicho fanya ila hapana nawaomba radhi kuwa ni bahati mbaya wakinizingua naingia ndani kama naogopa hivi kisha wakijaa mlangoni kama kawa nawapa shoti tuu watoto wadogo hawa hawana lolote.......

****"samahanini jaman naomba mnisamehe ni makosa tuu ila sio makusudi naomba mnisamehe kwa tatizo hili nisameheni  jaman ni bahati mbaya tuu.....ilikuwa ni sauti ya merry akiomba msamaha kwa wale watu ili ajue msimamo wao watafanyaje...ila na wao kwakuwa walishakuwa na mipango yao hata hawakupoteza mda ili waharibu wakaanza kumsogelea merry ili wamshike nae merry kwakuwa mipango yake iliendapowa akaanza kuondoka kuingia ndani kwake kisha akalock mlango kwa ndani kisha akawaandikia kwenye kikaratasi kwamba "ondokeni hapo kama mnataka amani" lakin bado tuu wakutoka pale mlango  Hawakutoka  kwa kujitia et wanataka kuvunja mlango ili waingie kinguvu mle basi nae baada ya kuona vile hakuchelewa akabonyeza batani yake ya remote ambayo ni kwaajili ya shoti na kweli baada ya mda watu wa pale nje walianza kulalamika kama mtoto kachapwa kwa kuonelewa na mtu ambae sio mzazi wake
....

Ben nae baada ya kuhihisi kukaa ameshachoka basi akajitoa kutoka kule chini ili aweze kuonana na merry alijaribu kutoka mlango ukawa umefunya akatafuta njia nyingine ya siri ambapo hiyo njia ya siri alipopita ghafla alijikuta akiwa nje kabisa, kupepesa macho kwa mbaaala akaona kama kuna kundi la watu wanamfata ben akapiga akili
''"duuh sasa hii shida hapa nkiludi ndani washanioa bora niwaenjoy nione nikidakwa basi...... Ben niliondoka mbio kutoka pale niliposimama kugeuka nyuma bado nikaona ninafwatwa tuu nikicheki mbele hakuna njia zaidi ya poli lililonisonga sikuwa na namna niliingia ndani ya lile pori huku nikiwa makini....

Huko nyuma nako wakawa bado wakimtafuta tuu ben ila baadae walisimama ili wajadiriana Watumie njia gan ambayo inaweza kuwa rahisi kunishika mmoja wao akasema hapa tukafuate pikipiki hata mbili zinatosha wakaona ni wazo la maana kwasababu hawajui niko wapi kwa mda ule hawakupoteza hata sekunde wakawatuma wenzao wawili ili wakafate pikpiki hizo huku wengine wakiendelea kusonga mbele kwa miguu....
     Upande wa ben nilikuwa nimetembea hadi nahisi miguu yangu kuzam tumboni daah sasa hili tatizo inamaana saizi mimi naishi kama mkimbizi maisha gani nilijisemea hivo baada ya  kujiona nmechoka sana ila sikukata tamaa eti wanikamate kisa nimechoka hapa nakufa kiume dadeki zao, nilijipa moyo gafla nguvu zikaja nikaanza tena kuchanja mbuga huku nikiwa napeleka miti pembeni ili niweze kupita kwa urahisi kufika mbele palikuwa na kamto sio kakubwa sana ila kana nyasi nyingi sana mwanzo nilitaka niruke ili niende upande wa pili halafu niendelee kukinbia ila roho ikasita nilipotulia nikasikia kama vishindo nyuma yangu ila nadhani walikuwa mbali kidogo niligeuka nyuma pengine naweza ona chochote ila sikuona kitu niliporudisha macho mbele niliweza kukutana na mzee mmoja akiwa katika mtumbwi wake anasafiri na mimi sikusita nikaomba lift yule mzee hakuwa mchoyo aliniambia njoo tuu kijana twende kisha akanisogezea hadi jirani na pale ambapo mimi ambapo nilisimama nilipanda tuliendelea na safari tulienda umbali mrefu nisijue tunaenda wapi ikafika sehem fulani kulikuwa ni eneo tulivu sana hapo ndipo mzee yule alisimamisha mtumbwi ule na kutaka nishuke nikajifanya kuleta nyodo akanambia jitie mpumbavu hivohivo haya maeneo yana mamba looh baada ya kusikia vile niliruka mwenyewe kwenye mtumbwi na kutua hadi pembeni kabisa, yule akacheka kisha akasema ahaaaa kumbe mwoga hivo eeeeh utaogopaje kitu kama mamba eti. Duuuh we mzee mchawi au inamaana we huogopi mamba kabisa nilimuuliza hivo nae akajibu siogopi ndio na ndo mana nmesafiri kwenye huu mto mana huu wote unamamba kama kumi kwa idadi yaani kutoka pale nilipokukuta hadi hili eneo....yule mzee alivoongea vile nilibaki nimemkodolea macho ila yeye aliendelea ni kweli tena hata usishangae mwingine yule pale angalia kwenye maji....mamaaaaaaa weeeee ni kelele nilizotoa baad ya kumwona mamba kwenye maji tuliyotoka
  Haya tuendelee na safari kijana au jee...ah sawa babu twende tuu ila usinifanyie ubaya wowote ule..aha bhana ee sa ubaya gani nikufanyie mimi tena wewe.. We kama huogopi mamba mtu mzuri kweli wewe sidhanii..haya kijana naweza kuwa msaada kwako lakini..sawa ntashukuru zilikuwa ni moja ya stori tulizokuwa tukiongea tunapotembea sio mda mwingi tukawa tumefika eneo moja ambalo lenyewe lilikuwa ni kubwa lina sehemu zenye milima kulikuwa na mto ambao maji yake yametuama kwenye mawe meupe na maji ni masafi
    Kijana jisikie upo kwenu tena uwe huru nilifurahi kwakuwa mazingira yake yalinivutia sana mana ni kama sehemu za wahindi ila ile nyumba ya mzee yule ilikuwa kama tempo zile ambazo mara nyingi ni kwa wachina ndio zinatumika......
.....jaman huyu ben hajatoka tuu we beniiiiiiiiii, beniiiiiiiii toka huk bhana dah alikuwa nj merry baada ya kuona myda inayoyoma na bado mimj sijatoka tuu aliniambia nijifiche alinitafuta bila mafanikio inamaana alitoka wakamfukuzia au mbona huu mlango upo wazi nani katoka baada ya kujiuliza maswali hayo akanyanyua simu yake na kumpigia ben simu iliita ikapokelewa lakini mazungumzo hayakuweza kuwafanya waelewane lugha kisha merry akaona isiwe shida akatuma meseji "we ben uko wapi au wamekukamata... Baada ya mda si mwingi ben akareplay hawajishika ila nadhani bado wananitafuta katika msitu mmoja hivi na mimi nipo mbali sana naomba tunza hivo natarajia ntakuja kurudi sio mda mwingi basi merry alipika na kula hatimaye mda wa kulala ulifika na kwa ben ndivyo ilivokuwa

::::::porini ilipofika asubuhi ben akiwa amelala aliamshwa na yule babu mida kama ya sa kumi na mbili hivi

"aaah babu nini kwa sauti ya kiuchovuchovu babu akasema acha kulala huu mda wa mazoezi hebu amka usipoamka nakuwekea ngee.... Ah sawa sawa sawa mzee naamka nge!!!! Ben nae akaamka kisha ...........itaendeleaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni