Jumapili, 28 Agosti 2016

De 21

Gangstar noma
By: benchrys
21

..oya we dogoooo hebu simama hapo nataka niongee na wewe baadhi ya mambo ya muhimu sana mdogo wangu------we dogo ben vipi inamaana hatusomani au unazingua bhana,,,, ilikuwa ni sauti ikiniita kutoka nyuma yangu sijui alikuwa ni nani maana sikuweza kumgundua hata kwa sauti tuu moyoni nikajisemea hata sitaki mazoea na mtu yoyote maana wanaweza nikwamisha safari yangu nikajikuta naishia tu njiani humuhumu,,,,, niliendelea kutembea lakini nikiwa natembea nisikia kishindo kikiwa kinatokea nyuma yangu tena nilitaka nigeuke lakini nikatumia tuu staili ya kuhisi kwa jinsi alivonielekeza kule porini basi haikupita muda nilihisi kama kuna mtu anataka kunishika begani lakini kabla  hajafanikiwa kunishika niligeuka na kumdaka mkono wake ndani ya nusu sekunde akawa ameinamia mbele hawezi kufanya chochote
        Oya mkono huo mwanangu hujui utauvunja acha upuuzi ukiona nimejitoa hapa wewe naumiza, alisema maneno yale yule jamaa ambae nilikuwa nimemshika mkono wake kwa kumzuia asiweze kufanya chochote kile,,,,, kwa hiyo wewe kwa ndoto zako unaota kwamba hapa unaweza kujitoa kirahisi tuu haya nambie shida yako ni nini na jina langu umelijulia wapi ukijitia mjanja huu mkono nauvunja jumla, nilimwambia hivo nikiwa bado na ule mkono wake ambao haukuweza kufanya chochote kile
M m iii sijaagizwaa na mtu kukutafuta kabla hajamalizia kuongea yale nilimpa kofi zito kisha nikamuuliza nani ka kwambia kuwa umeagizwa kumbe inaonyesha dhahiri kwamba umeagizwa sasa ndio utasema hebu twende acha ujinga niliahirisha hata safari ya kwenda nyumbani nikageuza nae kurudi kule kwa merry ilinikamshikirie aseme ukweli,,,,,,,,nilitembea nae kwa kuvutana hadi eneo moja hivi ambapo nikiwa naendelea kwenda walitokea vijana wawili wakiwa na nondo mikononi mwao na kuniamrisha oya mbona umemshika mwanetu kuna noma yoyote au mwachie basi sivyo tunakuzingua hapahapa,,, waliposema maneno hayo hata sikuwaza kumwachilia sijakaa vizuri kuna moja wao alinyanyua ile nondo na kutaka kunipiga nayo lakini kwa kutumia mkono mwingine niliidaka ile nondo na kuimfumua nayo mgongoni alianguka chini huku akiwa kama anavuta kamasi ishara ya kuonyesha analia kibishi sikujali hilo nilimfunga yule niliyemshika kisha nikamfuata yule mmoja ambae kwa  hapo alikuwa anatagfuta njia ili aweze kukimbia,,,,, kwakuwa niliachana nae kwa umbali fulani alipfika mbali alianza kunipa maneno ya kunitusi kwamba sikujali nikawa namfuata kumbe kulikuwa na nyumba jirani hapohapo akaingia kwenye moja ya geti ambalo lilikuwa jirani na kufunga nilikifanya nikachukua picha ya ile nyumba kwa kutumia simu kisha nikarudi kwa wale wengine nilifika nikambeba yule mmoja ambae bado anafahamu nikafika hadi kwa merry na kumpa kiti ok huu ndio mda wa wewe kunambia ni nani kawatuma kunuitafuta kwa kunifanya nimarafiki zangu ilimtume taarifa kwake,

Baada ya kuuliza bila kujibiwa nilikchukua waya mmoja na kuunga kwenye kile kiti na kumfunga kisha nikauliza tena hakujibu ila alicheka nikaona hizi ni dharau sasa nilichukua remoti na kubonyeza moja ya kitufe alilalama na kuanza kujieleza mwenyewe baada ya kuona anajieleza mwenyewe nikamfungua nakumwambia ok nakusikiliza ni nani kawatuma kwa kuogopa ile shoti ya umeme tena ilimbidi aeleze ukweli wote kwamba..

******kuna mzee mmoja hivi  alitukamata vijana ambao tulikuwa tunatoka mtaa mmoja na yeye alitufunga mda kama wa siku tano kwenye chumba ambacho kilikuwa kina picha yako ambayo iliandikwa wanted humo ndani tulikuwa tukiletewa kila kitu baada ya zile siku akatufungulia na kusema huyu mtu ambae mmemwona katika picha namhitaji nimwone akiwa ni mzima wakati wowote kuanzia sasa nimewapiga picha nyie wote wahiyo hamwezi kukimbiliamahali popote pale mtakuwa mkiondoka asubuhi nakurudi mda wa jion kila mtu akiwa na majibu yake kama mmemwona au lah, baada ya kuongea yale maneno akatupatia kiasi cha hela kila wetu na kusema atakae jaribu kutoroka atamtumia wanajeshi ili waweze kumkamata na kitendo kitakacho fanywa kwa huyo nadhani itakuwa ni mfano kwa wengine, sisi wote baada ya kusikia maneno yale tulikuw na woga na hatukuweza kumbishia kwa lolote lile ambalo alikuwa akiambia baada ya mda kidogo siku kama mbili akatupatia namba ya simu akidai kwamba ndio namba yako wote tukawa tunajitahidi kupiga ile namba kwa wakati tukiwa na muda maana kama salio simu zetu bada ya kutununulia aliunga kifurushi cha mwezi ili tusiishiwe muda wowote ndo maana ilikuwa juzi nilipiga simu ili nikupeleleze upo maeneo gani ilinimwambie aje kukuchukua,,,,, hayo yote yalikuwa ni maelezo ya yule kijana baada ya hapo nikamuuliza kwa hiyo wenzio ni akina nani hakusita akanitajia majina mengi sana ila nikapotezea nilimwambie aondoke na asijaribu tena huo upuuzi nilimfungulia na kumwacha aende zake

Nikiwa mtaani mida ya jioni nilionakundi la watu wakinifuata nikajifanya sijawaona kisha nikaanza kuondoka taratibu lakini hawakusita walinifuata tuu
;;;;;oya mbona tunafatiliaana mnamatatizo au na mimi au, niljihami hivo moja wao akasema kwa wenzao tunaongea nae nini sasa kazi ni moja tumnyakue tuu twendezetu kwamkuu baada ya mimi kusikia vile niliondoka mbio ili wapungue mmojammoja,,, na wao wakaaanza kunikimbiza ila spidi yao ilikuwa ndogo sana katika kukimbia

Baada ya kukimbia hadi kwenye ukuta mmoja niligeuka nyuma na kukuta wamebaki watatu,,,,, nikiwa naukaribia ule ukuta nilisogea jirani na ukuta ule nilidunda kisha nikajigeuza na kuwaachia mateke ya uso wawili kisha nikamsogelea yule mmoja kum-bamiza ukutani wote wakawa tayari wapo chini kisha nikaendelea na safari yangu ya kurudi homenikiwa naendelea kwenda mbele ulitokea mwanga mkali sana ambao ulikuwa ukiumiza macho haraka nikatoa miwani ya kuzuia mwanga mkali kisha nikaivaa nakubadili njia niliyokuwa nikiifata nikiwa naendelea kwenda kuna pikipiki ilikuja kwa kasi sana kidogo inipitie miguuni lakini nilidank na kuikwepa kisha aliyekuwa akiendesha akaenda kuanguka mbele baada ya mimi kuona kile kitendo sikumfuatilia nikaendelea kutembea niktafuta njia ya kurudi nyumbani mana hii mitaa nilikuwa nimgeni

Baada ya nusu saa nilikuwa nimeshaiona njia ya kuelekea nyumbani nikanyoosha njia ile ilinifikishe nyumbani kwa merry, kwa mbali niliona kama kuna watu wengine watatu wakiwa na nguo nyeusi zote na miwani, ningeweza kubadili njia lakini lakini hakuna chochoro ambayo mimi naifahamu kwenye huu mtaa maana hadi nilifika nilitembea usiku kwa usiku basi nilitembea hadi nawakaribia hawa watu wawili ambao wote niliweza kuona wakiwa wamebeba mabegi makubwa wastani niliwasalimia wote hawakujibu nikapita nikiwa naendelea kwenda mbele mara nikahisi nayemelewa mgongoni nilianza kama kukimbia nae akaanza kukimbia gafla bin vuu niliruka beki juu sana kisha nikawa nyuma yake,,, akiwa ameduwa nilimfumua teke zito ili kumwongezea safari yake aliburuzika kama gurudumu bovu kisha nilisogea na kumvua lile begi kuangalia ndani ya begi kulikuwa na bastola ndogo ndogo niliichukua na kuchana lilebegi kisha nikaondoka kuelekea nyumbani..

Nilimkuta merry akiwa amekaa tuu kipweke huku akibonyeza simu yake nilimsalimia kisha na mimi nikajiunga kuchezea simu, merry alisimama na kuwasha tv alipowasha tuu alikutana na habari ambayo hata hakutaka kuamini nakubaki amenitumbulia macho maana ilikuwa ni breaking newz

Ivi we ben hizi habari ni kweli au wanazingua tuu,,, ni swali ambalo lilitoka kwa merry baada ya kushngaa kwa muda mrefu akiwa haamini zile  taarifa za kwenye tv,,, habari ilisema.itaendeleaaaaaaaaaaaaaaaa

benchrys.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni