Gangstar noma
By: benchrys
24
...........niliishika vizuri ile miamba ya magoli kisha nikajizungusha ili kurudi upande wa pili hapo nikawa tayari nishawaangusha wawili alibaki mmoja. Alijifanya kidume kunisogelea mi nikawa nimesimama huku namcheki uwezo wake juu ya upambanaji, nilimsogelea huku mkono ukiwa mfukoni nae hakuchelewa akarusha teke mgongoni ila nikazidi kumsogelea tuu alijitahidi kuruka awezavyo ili anipige lakini ben nilizidi tuu kumfuata kasha nikatoa mkono mfukoni baada ya hapo alijaribu kurusha ngumi nikaudaka mkono kisha nikamvutia kwangu, alikosa balance nyie mnaita hivo sijui, tuendelee alipokosa balance ilimpelekea kupepesuka na mimi iliasiendelee nilinsindikiza na teke ili aendelee na safari yake hali ambayo ilimfanya akangukie mdomo nikajisemea aaaah potelea mbali mi sijui umetaka mwenyewe hayo yote yasingekuwapo baada ya hapo yule alikuwa akilia tuu na hawa waliopigwa na kuanguka mwanzo wakawa wananyuka mda huu baada ya kuona wananyanyuka nilijifanya kama sijawaona hivi nikawa kama naondoka hivi nao wakasemezana tukamvae kabla hajafika mbali,walikubaliana hivo kisha wakajipanga kuja kwa kasi ili wanivae tuanguke wote. Walitoka mbio kama mbwa wa jeshi kuelekea upande ambao mimi nipo waliponikaribia tu nilichumpa juu kisha nikatua nyuma yao na kuwabetua wote walitua chini kama mgomba ulioegeshwa tuu niliwaonea huruma nikaanza safari ya kurudi nyumbani......nilipitia pale ambapo nilirusha lile bagi ila nilipoingia tuu ndani nikakuta vijana wengine wawili huku wakiwa na mapanga kama ya kininja hivi, sikujali hayo yote nililifuata lile begi nikalivaa kisha nilianza kuondoka lakini kabla sijaondoka alikuja mmoja katika wale wawili huku akiwa kaelekeza lile panga kwangu, ni kitendo cha sekunde tuu nililidaka lile panga na kumshika asiweze kufanya chochote, nae baada ya kuona hana ujanja akamkonyeza mwenzie ili achukue hatua kwa kitendo kile. Lakini kabla ya kufikiria cha kufanya nikamwambia jitia mjinga mfe wote hapo kesi mimi siogopi hata kidogo kwahiyo ntafanya chochote hata weka hilo panga chini kabla sijamtanguliza huyu mwenzio mahali ambapo hatarudi,,,, hakuleta ubishi akaweka lile panga chini kisha akajifanya kama anasaluti kumbe alikuwa kaweka bastola iendayo kwa jina pisto nyuma ya mgongo wake nikiwa bado nimemshika yule mwenzake aliitoa ile pipe akaikoki lakini sikushituka ali pull triger kunielekezea mimi lakini wakati huo nilasha mgeuzia mwenzie ule upande kwahiyo alipopiga tuu risasi ilipenya moja kwa moja kwenye kifua cha yule mwenzie... Lahaura nini hiki sasa nimefanya alianza kujiuliza ni kitendo gani ambacho amekifanya "yaani nimempiga tena mwanangu duuh huu msala ntaeleza nini sasa"
mda huo yeye anaendelea kushangaa ben nilishaondoka na lile begi nakaribia nyumbani nikiwa bado njiani ilipita gari moja likiwa na mwendo wa kasi sana hadi watu wakasema watu gan hawa!!!! Kumbe walikuwa ni polisi wakielekea kule kwenye ile nyumba walikopigana watu akiwemo na Ben
****kumbe ule mda imelia risasi kuna mama mmoja alikuwa akipita pale aliposikia tuu ule mlio akapiga simu polisi ila kwa bahati polisi wamekuwa wazembe wakachelewa maana na mimi ningeshikwa
******we ben hilo begi lina nini mbona kama lina vyuma hivi ni vitu gani hivyo. Lilikuwa ni swali kutoka kwa naomi maana yeye mara huwa wa kwanza kuniona ninapoingia nyumbani,,
,,aha we lichukue kaliweke ndani mengine utajua badae. Alilipokea lile begi ili aende kuliweka ndani lilikuwa ni lile begi ambalo linasilaha za wale vijana watatu niliowaona kwenye vichochoro kule naomi akiwa anaelekea ndani.......haaaaa!!! Wewe ben umetoa wapi hivi vitu, kumbe naomi alilifungua lile begi ili ajue kilichopo ndani mule baada ya kukuta zile bastola ndogo ndio akatoa kelele za mshangao.. Baada ya kugundua kuwa kafungua nilipaza sauti na kusema: "naomi nimekwambia ukaweke ndani mengine mtajua baadae mbona hunielewi"
Naomi baada ya kusikia vile alipitiliza hadi ndani akaweka begi kisha akaendelea na mambo ya yake.
Nikiwa nimetulia simu ilianza kuita, ilionyesha jina la merry niliipokea
;;hallow mambo ben
;;powa tyu mzima ccta
;;mi niko powa. Halafu we ben
;;ndio mi ben vipi kwan
;;mbona unanyanyasa watu wa watu mtaani kisa ni nini,aliuliza hvo merry
;;sio kwamba nawanyanyasa ila wao ndio wananinyanyasa na lengo lao kuu ni kunikamata sasa mimi siwezi kukubali hilo swala hata siku moja eti nikamatwe kizembe bila hata sababu yoyote
;;haya bhana mimi nilikuuliza kupigana ulijifunzia wapi
;;daah na wewe ukitaka kujua kitu unakumbusha kwa juhudi kweli....
;;ni lazima nikumbushe aya niambie saizi
;;haya bhana ila mbona kuna mishe naifanya na hii habari sio fupi tufanye unitafute baadae au jee
;;dah pow bhna saa mbili ntakutafuta tuu kwaheli
;;powa
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya mimi na merry akitaka nimwambie nilikojifunza kupigana wakati mimi babu alinikataza kumwambia mtu yeyote
.
.............................
Ivi huu sasa ni utani hivi inawezekanaje kile kidogo kuwapiga eti hadi mmeumia hivi inamaana...yani siwaelewi kabisa kumbukeni anazidi tuu kukusanya silaha zenu na msipokaa vizuri mtajikuta mnaozea jera endeleeni na huo uzembe mimi mkikamatwa sitajua na msinitaje maana atakae nitaja nampeleka kuzimu bila kutoa taarifa huko, halafu wenzenu watatu wako wapi mbona mpo wachache hii leo. Boss hata sisi hatujui maana waliondoka na kusema wanaenda sehemu fulani wamesikia kuwa beni yupo huko....huyu akiwa anaendelea kuongea simu ya boss iliita
;;hallo nani mwenzangu
;;unaongea na mkuu wa kituo cha polisi fulani(alimtajia jina) samahani unajika kufika hapa si zaidi ya dakika tano..kisha simu ilikatwa
Hivi haya ni mambo gani kituoni kuna nini mbona nachanganyikiwa anyway let me follow. Baada ya kuongea vile huyo wanaemwita boss alitoka katika jumba la kifahari hilo akachukua funguo za gari na kuelekea kwenye gari mojawapo kisha akaliwasha na kuondoka nalo******huku nyuma
Wafanyakazi wote walikusanyana na kujiwekea mipango ya kutoroka, walikubaliana wote bila hata kipingamizi cha upande wowote, walifungasha kila kilicho chao na kinachoweza kuwasaidia huko mbele maalumu kwa kuanza safari lakini walipofika geti kubwa la kutokea nje walijaribu kuvuta bila mafanikio wakajipanga kuwa walivunje baada ya hapo walijisogeza wote na kuanza kulipush lakini bado ikawa zero tuu ila kuna mmoja wao alipoangalia sehem akaona funguo aliiokota na kusogea hadi kwenye lile kufuri na kuchomeka ile funguo alipoizungusha kidogo tuu kufuri lilifunguka bila ubishi wakachukua mabegi ili watoke watembee zao ila walipofika tuu nje walishangaa kuona gari kubwa limepack vizuri sehemu ya kutokea na muda si mrefu walitokea polisi. sijui walijificha wapi hata sijui. Wote wakiwa na mabegi yao waliamrishwa waingie kwenye lile gari na hakuna aliyeweza kuleta ubishi wowote****** hilo ni janga lililotokea kwa wafanyakazi na boss aliyewaajili watu wamtafute ben
...........huko polisi baada ya boss yule kuulizwa maswali hakuna aliloweza kulijibu kwa kujitetea kwa akapelekwa gerezani na wafanyakazi wake(hivi ina maana hawa hawana hata idea ya kuwa nimefunfwa yaani hata mdhamana tuu hawaji kuleta duuh hii too much)alikuwa akijisemea yule boss pekeyake kule gerezani.
Ngrrrrrrrrr ngrrrrrrrr ngrrrrr huo ulikuwa ni mlio wa simu yangu aina ya Samsung ikiita niliitoa nfukoni na kuipokea lakini sikuongea chochote maana namba ilikuwa ni ngeni kwahiyi ikaniwia shida kuongea lakini cha ajabu nae hakuongea hadi simu ilikata
..upande wa pili..huyu boya mbona haongei ili tumrekodi ahh achana nae huyo tuendelee na yetu.
Nikiwa nimetulia tena simu yangu iliweza kuita tena nilipoangalia ile namba nikajisemea daaaah mambo gani haya atha alikuwa ni......itaendeleaaaaaa
benchrys.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni